Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Muundo mpya wa uchoraji wa ukutani (jadariya) katika Uwanja wa Palestina katikati ya mji mkuu wa Iran, Tehran, umewekwa hadharani sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kuuawa Shahidi Jenerali Qasem_Soleimani. Ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya Kiebrania unasema: “Kila siku mnazidi kukaribia saa ya kutoweka.”
Ujumbe huu wa kiishara unaakisi msimamo wa mhimili wa mapambano na kusisitiza kuendelea kwa njia na fikra za shahidi Soleimani katika kukabiliana na ubeberu na uvamizi.
Uchoraji huu ni sehemu ya mfululizo wa kazi za kisanaa zinazobeba ujumbe wa kisiasa na kitamaduni, huku ukihifadhi kumbukumbu ya viongozi wa mapambano kama alama ya kusimama imara na uthabiti.
Your Comment